Tuesday, May 11, 2010
Hukumu Tucta leo, Wizara tano zakutano kunusuru mgomo
BARAZA kuu la Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (Tucta) linakutana leo kujadili hatma ya mgomo wa wafanyakazi ulioahirishwa kusubiri mazungumzo na serikali.Kikao hicho kinaitishwa siku tatu baada ya serikali kukutana na wajumbe wa shirikisho hilo kujadili madai ya wafanyakazi, ikiwemo suala la nafuu ya kodi inayokatwa kwenye mishahara.
Katika mkutano huo uliofanyika Jumamosi iliyopita, serikali iliwakilishwa na makatibu wakuu kutoka wizara tano kuzungumzia suala hilo lililoongeza utata baada ya Rais Jakaya Kikwete kuingilia na kutoa tamko la kubatilisha mgomo, huku akiwaita viongozi wa Tucta kuwa ni "waongo, wazandiki, wanafiki na wafitini".
Wizara ya Wizara ya Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana, wizara ya Fedha na Uchumi na Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma ni miongoni mwa wizara hizo zilizoshiriki kujadili madai matatu ya wafanyakazi hao ikiwemo nyongeza ya kima cha chini cha mishahara.
Akizungumza katika mahojiano maalumu jana, kaimu katibu mkuu wa Tucta, Nicholaus Mgaya alisema ripoti ya mkutano huo ndio itayotoa mwelekeo katika kikao cha leo kuhusu mgomo huo.
"Leo ndio tutajua wafanyakazi wagome au wasigome baada ya wajumbe kuipitia kwa undani ripoti ya kikao cha Jumamosi," alisema Mgaya.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment