Raia wa Kenya Nathan Mtei anayetuhumiwa kumleta nchini mlemavu wa ngozi(albino) Robinson Mkwana Mnyoti ili kumuuza jijini Mwanza.
BAADA ya wimbi la mauaji ya albino kwa ajili ya kuuza viungo vyao kudhibitiwa na Jeshi la Polisi nchini, mbinu za wauaji zimebadilika na sasa wameanza kuwauza wakiwa hai. Hali hiyo imedhihirika baada ya polisi mkoani hapa kufanikiwa kumnasa raia wa Kenya akituhumiwa kumsafirisha albino kutoka nchini mwake hadi jijini hapa kwa lengo la kumuuza. Mkenya Nathan Mtei (28) hivi sasa anashikiliwa na Jeshi hilo mjini Mwanza kwa tuhuma za kumsafirisha binadamu mwenzake, albino Robson Mkwana Mnyoti (20) kwa lengo la kumuuza. Kamanda wa Polisi wa Mkoa Simon Sirro, jana alithibitisha tukio hilo na kusema, “ni kweli wanamshikilia Mtei tangu Agosti 15 mwaka huu alipokamatwa saa 10 jioni.
No comments:
Post a Comment