Tuesday, May 11, 2010

Sendeka, Shekifu wakalishwa kitako !


WAZIRI Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Bw. Shamsi Vuai Nahodha amewataka Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Bw. Henry Shekifu na Mbunge wa Simanjiro, Bw. Christopher Ole Sendeka kuweka kando tofauti zao binafsi wanapotekeleza majukumu yao ya kutumikia wananchi.

Akihutubia wananchi wa mji mdogo wa Mererani wilayani Simanjiro juzi katika mkutano wa hadhara uliohudhuriwa na viongozi hao, Bw. Nahodha aliwakumbusha viongozi hao kuwa penye migogoro ya wenyewe kwa wenyewe hakuna mafanikio.
Bw. Shekifu na Bw. Sendeka waliripotiwa kukwaruzana walipokuwa kwenye kikao cha ndani katika Kijiji cha Sukro wilayani Simanjiro baada ya Sendeka kupinga amri ya mkuu huyo wa mkoa ya kumtoa nje ya ukumbi wa mkutano huo.

Katika tukio hilo, mkuu wa mkoa alidaiwa kutishia kumsweka rumande mbunge huyo kwa saa kadhaa kutokana na madaraka yake, hata hivyo viongozi hao wanadaiwa kumaliza tofauti zao.

No comments:

Post a Comment