Tuesday, June 8, 2010

Kocha raia wa Denmark Kuinoa Taifa Stars!


KITENDAWILI cha nani atakuwa Kocha Mkuu wa Taifa Stars kimeteguliwa, ambapo raia wa Denmark Jan Poulsen mwenye umri wa miaka 64 amepewa jukumu hilo. Kocha huyo aliyepata kuzinoa timu za Taifa za Singapore, Jordan na Almenia kwa nyakati tofauti atasaini mkataba wa miaka miwili kuinoa timu ya Taifa ya Soka ya Tanzania ‘Taifa Stars’ kuanzia Agosti mwaka huu akirithi mikoba ya Mbrazil, Marcio Maximo. Akizungumza Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Fredrick Mwakalebela alisema uamuzi wa kumteua Poulsen ulifikiwa juzi kwenye kikao cha Kamati ya Utendaji ya TFF chini ya Rais wa Shirikisho hilo, Leodegar Tenga. Wasifu wa kocha huyo mpya unaonesha kuwa ni mchezaji mstaafu wa kimataifa wa Denmark, ambapo akiwa Kocha Msaidizi wa timu ya Taifa ya nchi hiyo, alitwaa ubingwa wa mataifa ya Ulaya katika fainali za mwaka 1992, ambapo timu hiyo iliifunga Ujerumani katika fainali. “Mwaka 2007 akiwa Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Jordan, Poulsen aliiwezesha timu ya umri wa miaka 20 ya nchi hiyo kufuzu kwa fainali za Dunia zilizofanyika Canada. “Kati ya mwaka 1992 na 1999 Poulsen alifundisha timu ya Taifa ya Denmark ya umri chini ya miaka 19 na pia amefundisha timu ya Taifa ya nchi hiyo ya chini ya umri wa miaka 21,” alisema Mwakalebela akielezea wasifu wake. Alisema Poulsen si tu ni kocha bali pia ni Mkufunzi wa Walimu wa Soka wa kiwango cha Kimataifa anayetambuliwa na Shirikisho la Kimataifa la Soka (FIFA) na amekuwa akiendesha mafunzo yanayoandaliwa na shirikisho hilo kwa nchi mbalimbali

No comments:

Post a Comment